Skip to main content

WAKULIMA WATAKIWA KUTUMIA TEKNOLOJIA YENYE TIJA ,ILI KUPATA MAZAO YENYE BORA




mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro,wakati akiofungua Maonyesho ya zana za kilimo katika viwanja vya Taasisi ya Utafiti wa kilimo ya Seliani 




Afisa mauzo wa kampuni ya Irrico Saimoni Manyike akimuelewesha mkulima jinsi kampuni yao inavyofanya kazi ya kusambaza teknolojia ya umwagiliaji wa Matonye



Washiriki ambao ni wakulima wakifuatilia kwa makini mada ambazo zilikuwa zikiendelea wakati wa ufunguzi






Habari picha na Woinde Shizza,Arusha




sekta ya kilimo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ufugaji holela , ambao hupelekea uharibifu wa mazingira,Teknolojia duni pamoja na ugumu wa kupata mitaji ya kuboresha miundombinu ya kilimo. 


Hayo yamebainishwa na mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro,wakati akiofungua Maonyesho ya zana za kilimo katika viwanja vya Taasisi ya Utafiti wa kilimo ya Seliani vilivyopo ndani ya jijini Arusha ambapo ni mara ya kwanza kufanyika .

Alisema kuwa sekta ya kilimo inakabiliwa na changamoto za ufugaji holela ambao unasababishwa na wafugaji ,wakulima kutumia teknolojia duni au zazamani katika ukulima pamoja na wakulima wengi kukosa mitaji ya kubesha miundo mbinu ya kilimo

Alisema kuwa hii inachangia kwa kiasi kikubwa kukwamisha maendeleo ya sekta hii kutokana na wananchi wengi kutumia kilimo cha kawaida badala yakutumia kilimo cha kisasa ambacho kinaleta tija .


“hapa Tanzania zaidi ya asilimia 75% wanategemea kilimo lakini kati yao n asilimia 1.5 tu ndio wanatumia kilimo cha kisasa kama kilimo cha umwagiliaji ,kupanda mbegu bora pamoja na kilimo cha matone hivyo ni vizuri wakulima wetu kujitaidi kutumia kilimo cha kisasa ili kuweza kufanya kilimo chenye tija ambacho kinamnufaisha yeye mkulima mwenyewe na kuachana na kilimo cha kawaida au naweza sema cha kienyeji”alisema Daqarro

Alisema kuwa watanzania tunauwezo wa kuzalisha mazao bora kwakuwa tuna aridhi nzuri ,maji mengi ya kutosha tunayo kwani tunamito mingi inayotoa maji hivyo tukiamua kuwekeza na kulima kilimo chakisasa tunaweza kusaidika na hata pato la mkulima litakuwa na sio mkulima tu na pia pato la serikali pia litaongezeka kutokana na kilimo.

Aidha mkuu huyo wilaya alisea kuwa serikali inawashukuru wadau kwa kuupa mkoa wa Arusha heshima ya kufanyika kwa maonyesho hayo ambayo yatafanyika kwa muda wa siku mbili hivyo amewataka wananchi wajitokeze kwa wingi katika kujifunza teknolojia mpya za kilimo na ubunifu wautaalamu mbalimbali .

“napenda pia kuwataka waonyeshaji kuangalia suala la bei kwani asilimia 75-80 ya wakulima ni wakulima wadogowadogo hivyo ni vyema wakauza bidhaa zao kwa bei nafuu ili wakulima wa hali ya chini aweze kumudu kununua bidhaa ili waweze kuendana na kasi ya kilimo cha kisasa ,Serikali kwa kushirikiana na wadau wa kilimo wanaangalia ni kwa namna gani 

wataweza kuboresha sekta hii ya kilimo kwa kutoa elimu mbalimbali kwa wakulima ili kuepukana na kilimo duni ambacho kinasababisha hasara kwa wakulima nchini”alisema Daqorro

Kwa upande wake mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti ya Seliani Dr Daniel Mafuru amesema kuwa wamekua wakishirikiana na wadau mbalimbali wa kilimo, katika uzalishaji wa Teknolojia ,pamoja na kuwatafutia wadau wa kilimo masoko ya mazao yao.

Aidha alisema kuwa Seliani wapo tayari kuwaunganisha wakulima na waonyeshaji wa teknologi ,ilikuwawezesha wakulima kupata mafunzo na kubadilishana ujuzi pia iwapo watauwaunganisha itawasaidia kufahamu namna ya kuhifadhi mazao yao baada ya uvunaji ili wasipoteze mazao kama ilivyokuwa kabla ya kupata elimu hiyo ya kilimo.

Kwa meneja masoko wa kampuni ya John Deere ambaye pia ndio wadhamini wakuu wa maonyesho haya Wayne Travas alisema kuwa kampuni yao zinatefaya kazi ya kuwaletea wakulima wadogo mashine za kilimo ambazo zitawasaidia kufanya kazi vizuri na kwa teknologia za kisasa pamoja na ubora mwingi.










mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti ya Seliani Dr Daniel Mafuru Akifafanua jambo wakati wa ufunguzi wa maonyesho hayo



Washiriki wakifuatilia







meneja masoko wa kampuni ya John Deere ambaye pia ndio wadhamini wakuu wa maonyesho haya Wayne Travas Akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari



katika maonyesho haya pia kamera yetu iliweza kumkuta mwimbaji mashuhuri wa jijini hapa Nakaya Sumari akiwa na Phidesia Mwakitalima nao pia waliuthuria katika maonyesho hayo ili nao waweze kulima kilimo chenye tija 



Baaadhi ya wakulima wakiangalia matrekta ya kisasa yanayouzwa na kampuni ya John Deere nambao ni wathamini wakuu







Mmoja wa mkulima akiangalia jinsi ngowe zilizolimwa kwa njia ya matone zilivyostawi shambani



Afisa mauzo wa kampuni ya Irrico Saimoni Manyike akiwaonyesha wakulima hawapo pichani jinsi kilimo cha umwagiliaji wa mtone kinavyokuwa 













Mshauri wa sekta ya kilimo na ufugaji David Nyange akifafanua jambo katika uzinduzi wa maonyesho hayo 












Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...