Skip to main content

WANAWAKE WATAKIWA KUJIJENGEA TABIA YA KUPIMA AFYA ZAO







Na Woinde Shizza, Arusha

Wanawake wote hapa nchini wametakiwa kujijengea tabia ya kupima afya zao mara kwa mara ili kuweza kujua matatizo ya mwili waliyonayo na kuyatatua kabla ya madhara makubwa kutokea .

Hayo yamebainishwa leo na mkurugenzi wa kampuni ya Phide entertaiment Phidesia Mwakitalima wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu ya maandalizi ya wiki wanawake duniani ambayo inatarajia kuanza March mbili ambapo kwa mkoa wa Arusha maadhimisho hayo yanatarajiwa kufanyika kwa muda wa siku saba katika viwanja vya kumbukumbu ya sheikh Amri Abeid .

Alisema kuwa wanawake wengi wamekuwa awana tabia ya kupima afya zao mara kwa mara kitu ambacho ni hatari mno kwani maisha ya sasa ukilinganisha na hali ya tabia nchi ilivyo pamoja na vyakula ambavyo vinaliwa kwa kipindi hichi.

Alisema kuwa kutokana na tatizo hilo kuonekana hivyo kampuni ya Phide entertaiment wameamua kuandaa kuandaa maadhimisho haya kwa kuwapa fursa wanawake kujitokeza kupima afya zao bure ambapo alisema tukio zima litafanyika katika viwanja vya kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid kwa muda wa siku saba ambapo alisema kuwa maadhimisho haya yataanza rasmi March 2 hadi March nane.

" tamasha hili kubwa linawapa fursa wanawake kuweza kupima Afya yako bure na magonjwa ambayo yatapimwa katika wiki hii ni pamoja na Moyo, Kisukari, Macho, na figo hivyo napenda kuwasihi wanawake wenzangu wote wajitokeze kwa wingi waje wapime afya zao na wajijue vizuri "alisema Phide.

Aidha alisema kuwa mbali na kupima afya pia wiki hiyo itatumika kwa ajili ya kuwapa wanawake ushauri juu ya kupima afya zao mara kwa mara ambapo watawapa elimu ya kutosha .

"unajua kipindi hichi wanawake wamekuwa wanapata magonjwa ya haina mbalimbali na wingine wamekuwa wanapuuzia kwenda hospitali kupima afya zao mara kwa mara hivyo tamasha hili la wiki nzima litatumika kuwaelimisha wanawake faida za kupima afya zao mara kwa mara"alisema Phide.

Alimalizia kwa kuwataka wanawake wote kutopuuzia wiki hiii kwani ni muhimu sana kwa kujotokeza kupima afya zao na wajue mfumo mzima wa miiili yao ilivyo pamoja na kupata ushauri kutoka kwa wataalamu wa afya .

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...