Skip to main content

MBUNGE WA MAFINGA MJINI AKABIDHI MADAWATI



MBUNGE wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi akikabidhi madawti kwa viongozi wa kata ya sao hill kwa ajili ya matumizi ya shule 


MBUNGE wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi akipongezwa na viongozi wa kata ya sao hill kwa jitihada wanazozifanya kuleta maendeleo katika jimbo la mafinga mjini

Chumi alikabidhi mabati 80 kwa ajili ya kupauwa majengo hayo,mifungo 10 ya saruji,madawati 150 kwa shule za msingi za Ifingo na Kinyanambo

Na Fredy Mgunda,Mafinga. 



MBUNGE wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi ameendelea kutatua changamoto mbalimbali za jimbo hilo kwa kufanya ziara kwenye baadhi ya shuleza msingi zilizopo katika mjini wa mafinga na kukagua baadhi ya miundombinu inayoendelea kukarabatiwa kwa lengo la kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi wake.


Katika ziara hiyo Chumi alikabidhi mabati 80 kwa ajili ya kupauwa majengo hayo,mifungo 10 ya saruji,madawati 150 kwa shule za msingi za Ifingo na Kinyanambo ambayo yalitolewa na wakala wa shamba la miti Sao Hill huku chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Mafinga Mji kupitia mwenyekiti wake Yohanes Cosmas wakichangia mifuko 10 ya saruji kwa ajili ya kuunga mkono jitihada za mbunge za kukamilisha ujenzi wa miundombinu hiyo.


Katika hatua nyingine mbunge huyo alitembelea jengo jipya la ukumbi wa kisasa lililojengwa na kikundi cha Agape group ambalo lipo kwenye kata ya Kinyanambo kwa lengo la kuinua kipato cha halmashauri hiyo.


Baada ya mbunge kuona jitihada hizo alichangia 300,000 huku chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ikichangia 100,000 kwa ajili ya kumalizia ujenzi huo. 


Shule ya Msingi Ifungo iliyopo wilayani Mafinga inakabiliwa na changamoto ya miundombinu ikiwamo Umeme,maji ya bomba, madawati na nyumba za walimu jambo ambalo limedaiwa kuwa kukosekana kwa umeme limesababisha wanafunzi kushindwakufaulu vizuri.


Kilio hicho kimetolewa mwishoni mwa wiki na walimu mkuu wa shule hiyo Tedy Captein wakati akizungumza mbele ya mbunge wa jimbo hilo Cosato Chumi (CCM) wakati mbunge huyo akiwa kwenye ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo ya jimbo hilo.


Mwalimu Captein alisema baada ya rais John Magufuli kutoa elimu bure wanafunzi wameongezeka na hivyo wanahitaji maji safi ya bomba badala ya kuelendela kutumia maji ya tanki ambayo sio rafiki sana kwa wanafunzi hao.


Hata hivyo kutokana na ongezeko la wanafunzi wananchi wameamua kutumia nguvu kazi yao kwa kujenga jengo la darasa moja pamoja na ofisi ya mwalimu kwa gharama y ash.Mil. sita hadi kufikia kwenye lenta lakini walishindwa kumalizia.



Akijibu kilio cha shule hiyo kuhusu umeme mbunge Chumi alianza kwa kusema “Tutazungumza na shirika la umeme tanesco ili waweze kutuletea umeme ambao utasaidia kuongeza ufaulu wa wanafunzi wa shule hii.”alisema Chumi.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...