Skip to main content

JENGO LA OFISI YA JUMUIYA YA HIFADHI YA WANYAMAPORI WAG YA ZINDULIWA


Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Wizara ya Maliasili na Utalii Profesa Alexander Songorwa (kulia) akikata utepe kwa kusaidiana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Waga, Amon Kisinga wakati wa uzinduzi wa jengo la ofisi ya jumuiya hiyo uliofanyika katika Kijiji cha Nyakadete wilayani Mbarali, mkoani Mbeya jana. (Picha na Friday Simbaya)



Mwenyekiti wa Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyapori Waga, Amon Kisinga anaiomba serikali kusaidia tatizo la mgogoro wa mpaka uliopo kati ya Jumuiya hiyo na Kijiji cha Ulata ambao unakwamisha shughuli za ulinzi wa wanyamapori kwa kuzingatia kuwa ni eneo muhimu kwa uhifadhi.

Alisema kuwa Waga ni asasi inayovutia iliyojaliwa vivutio vingi vya utalii na hii ilithibishwa zaidi na utafiti wa mambo ya wanyamapori uliofanywa na shirika la jamii la kuhifadhi wanyamapori (WCS) mnamo mwezi Mei mwaka 2015.

Kisinga alishukuru shirika la hifadhi la WCS kwa kuwajengea ofisi ambayo itakayosaidia kuendelea kupambana na vitendo vya ujangili.

Alisema kwa WCS wamekuwa bega kwa bega katika mchakato wa uanzishwaji wa jumuiya hiyo tangu mwaka 2008, hadi kuidhinishwa kwake mwaka 2015 na kupata hati ya matumizi ya wanyamapori (user right) mwaka 2016.

Kisinga alisema kuwa WCS walisadia kuwaunganisha na taasisi zingine zinazopambana na ujangili kama vile Hifadhi ya Taifa ya Ruaha (RUNAPA) na Kikosi maalum cha kupambana na ujangili (KDU), kanda ya Iringa.

Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Waga, ina ukubwa wa eneo km za mraba 315 na inaundwa na jumla ya vijiji vitano ambavyo ni Nyakadete, Nyamakuyu, Igomaa, Ihanzutwa na Mahuninga, vyote vikiwa na nia ya kulinda na kusimamia rasilimali za wanyamapori kwa matumizi endelevu.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Profesa Alexander Songorwa amewataka wananchi waishio kandokando mwa maeneo yaliyohifadhiwa kutorubuniwa na waharifu kwa kushiriki vitendo vya ujangili.

Alisema kuwa wananchi kamwe msikubali kurubuniwa na kutumika katika uharifu huo kwani kuathiri mchango wa rasilimali kwenye uchumi wa taifa, na kuongeza kuwa kwa kufanya hivyo kunawanufaisha waharifu wachache wakati wanajamii wakiendelea kukosa mapato na huduma za kijamii.

Profesa Songorwa aliyasema hayo wakati akizindua jengo la ofisi ya jumuiya ya hifadhi ya wanyamapori ya Waga uliyofanyika katika Kijiji cha Nyakadete wilayani Mbarali, mkoani Mbeya jana.

“kwa miaka ya hivi karibuni nchi yetu imeshuhudia ongezeko la ujangili na miongoni mwa sababu zinazochangia ni kukua kwa soko la meno ya tembo nje ya nchi yetu hususani mashariki ya kati na bara la asia; mmomonyoko wa maadili kwa baadhi yetu, vitendo vya rushwa vinavyosababisha wananchi wa kipato cha chini kurubuniwa na kujiingiza kwenye ujangili pamoja na ukiukaji wa sheria ya uhifadhi,” alisema Profesa Songorwa.

Alisema kuwa pamoja na ujangili kumekuwa na ongezeko la uvamizi wa maeneo yaliyohifadhiwa kwa ajili ya uchungaji mifugo, kilimo, uchimbaji madini na kuanzisha makazi.

“Haya yote huambatana na uchomaji moto na ukataji miti, vitendo vinavyosababisha uharibifu wa mazingira, ukiwemo uharibifu wa vyanzo vya maji,” alisisitiza Profesa Songorwa. 

Alisema kuwa kuongezeka kwa migogoro inayosababishwa na wanyamapori wakali na waharifu huchangiwa kwa kiasi kikubwa na watu kutoheshimu mipaka kwa kuvamia maeneo yaliyohifadhiwa au kusogea kabisa na maeneo ya wanyamapori.

Aidha, Mkurungenzi huyo wa Idara ya wanyamapori kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii alitumia nafasi kushukuru shirika lisilo ya kiserikali la WCS na wafadhlii wao USAID kwa kuijengea Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Waga jengo la ofisi kutakakosaidia kupunguza ujangili.

Alisema kuwa serikali kama mdau mkubwa wa uhifadhi itaendelea kujenga uelewa na kuwahamasisha wananchi na wadau wengine kushiriki uhifadhi hususan kuwaokoa wanyamapori walioko hatarini kutoweka kama vile tembo, faru, mbwa mwitu na wengineo.

Jumuiya ya Uhifadhi ya wanayamapori ya Waga (CWMA) ni moja ya Jumuiya ya Uhifadhi za wanayamapori 22 zilizopo Tanzania.

Waga inaundwana na vijiji vitano kutoka katika wilaya tatu, ambavyo ni Nyakadete na Nyamakuyu (wilaya ya Mbarali, Mbeya), Igomaa na Ihanzutwa (Wilaya ya Mufindi, Mkoa wa Iringa ) na Mahuninga (Wilaya ya Iringa, Mkoa wa Iringa)

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...