Skip to main content

TGNP: BAJETI YA ELIMU YA MWAKA 2017/2018 HAIJATOA KIPAUMBELE KWA MTOTO WA KIKE








Ofisa wa Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP), Veronica Magayane akitoa mada wakati wa mkutano wa uchambuzi wa bajeti ya wizara hiyo kwa mlengo wa kijinsia uliofanyika jijini Dar es Salaam jana.









Wadau wakiwa kwenye mkutano huo.



Mkutano ukiendelea.



Uchambuzi wa bajeti hiyo ukiendelea.



Mzee Hamisi Katumwa akichangia jambo kwenye mkutano huo.



Mdau Msafiri Mtakatifu akichangia jambo.



Mdau Wilfred akichangia jambo kuhusu bajeti hiyo.



Bi. Ester Tibaigana akichangia jambo.



Muonekano wa chumba cha mkutano huo wakati wa uchambuzi wa bajeti hiyo.



Bi. Marytaus Mbawala akichangia mada.


Na Dotto Mwaibale



MTANDAO wa Jinsia Tanzania (TGNP) umesema bajeti ya mwaka 2017/2018 ya Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi iliyopitishwa na bunge haijatoa kipaumbele kwa mtoto wa kike.



Hayo yalibainishwa na Ofisa wa TGNP, Veronica Magayane wakati akitoa mada katika mkutano wa uchambuzi wa bajeti ya wizara hiyo kwa mlengo wa kijinsia uliofanyika jijini Dar es Salaam jana.


Alisema licha ya bajeti hiyo kupitishwa na bunge haijaangalia changamoto zinazomkabili mtoto wa kike kama umbali kutoka makazi na shule, kiwango cha walimu kisicholizisha, kutokuwepo kwa mabweni ya watoto wa kike, kufanyishwa kazi nyumbani kwa walimu kama kuchota maji na kuwapakia walimu.


Alitaja changamoto zingine ni kukosekana kwa maji ambapo kumechangia kuwafanya watoto hao wa kike kuwa katika wakati mgumu hasa wanapokuwa kwenye hedhi.


"Changamoto hizi zote zimesababisha elimu kwa mtoto wa kike kushuka na kupelekea wengi wao kutofikia ndoto zao" alisema Magayane


Alisema matatizo mengi ya miundombinu ambayo huathiri zaidi watoto wa kike yanatokana na changamoto za mfumo wa bajeti ya sekta ya elimu hivyo suala la kuboresha miundombinu ya shule linapaswa kuwa kipaumbele zaidi kwa kuongeza fedha za bajeti ya maendeleo.


Akichangia katika mjadala huo, Mzee Hamisi Katumwa alisema kuna kila sababu ya kutenganisha Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) na Wizara ya Elimu ili kupunguza kutupiana mpira ambapo kumekuwa na ucheleweshaji wa maamuzi ambapo mtu akienda Tamisemi anaambiwa suala hilo ni la wizara na akienda wizarani anaambiwa ni la Tamisemi.


Msafiri Mtakatifu alisema kwa wakati huu kipaumbele kinachopaswa kutiliwa mkazo zi barabara za juu wala ununuzi wa ndege bali ni elimu kwanza mambo mengine yafuate baadae.


Gilbert Nelson alisema ili kuinua elimu inatakiwa wizara hiyo kutengewa bajeti ya kutosha na kuwepo na uwekezaji mkubwa kama serikali inavyofanya katika maeneo mengine.


"Hatuwezi kuingia katika uchumi wa maendeleo ya viwanda bila ya kuwa na watu wenye elimu" alisema Nelson.


Mwaka 2016/2017 katika bajeti ya Wizara ya Elimu iliidhinishwa shilingi bilioni 277 sawa na asilimia 31 ilikadiriwa kukusanywa kutoka kwa wahisani na washirika wa maendeleo.


Katika mwaka huu wa fedha wa 2017/2018 serikali imekadiria kukusanya kutoka kwa wahisani na washirika wa maendeleo shilingi bilioni 310 sawa na asilimia 33.7 ya fedha ya maendeleo ikiwa ni ongezeko la utegemezi kwa asilimia 10.6.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...