Skip to main content

MAOFISA UGANI WATAKIWA KUTUMIA MAFUNZO WANAYOPATA KUWAELIMISHA WAKULIMA




Mtafiti, Bestina Daniel kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), akizungumza na maofisa ugani wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku moja kwa maofisa hao kutoka kata zote na vijiji vya wilaya hiyo Mkoani Tabora leo. 






Ofisa Kilimo wa wilaya hiyo ya Uyui, Deogratius Mwampinzi, akizungumza katika mafunzo hayo. Kushoto ni Ofisa Kilimo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora, Said Babu.



Ofisa Kilimo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora, Said Babu akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo.



Mshauri wa Jukwaa la Bioteknolojia (OFAB), Dk. Nicholaus Nyange akitoa mada kwenye mafunzo hayo.

Mtafiti wa mazao ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ukiriguru, mkoani Mwanza, Bakar Japhet akitoa mada.


Mtafiti wa pamba kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ukiriguru, mkoani Mwanza, Stellah Chilimi akitoa mada.



Maofisa Ugani wa wilaya hiyo wakiwa katika mafunzo.



Mafunzo yakiendelea.



Taswira ya chumba cha mafunzo.



Maofisa ugani wakiwa kwenye mafunzo hayo.






Maofisa Ugani ndani ya mafunzo.





Wanahabari waliopo kwenye ziara hiyo ya mafunzo wakiwa kazini.





Mtafiti, Bestina Daniel kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), akiteta jambo na ofisa mwenzake, Teddy Lyimo.




Na Dotto Mwaibale, Uyui




WATAALAMU wa kilimo wa Wilaya ya Uyui mkoani Tabora wametakiwa kupokea mafunzo na kuyapeleka wa wakulima ili kuwasaidia kupata mbinu mpya za uzalishaji na zinazotumia teknolojia katika kuongeza tija kwenye uzalishaji wa mazao mbalimbali yanayolimwa kwenye maeneo yao.




Kauli hiyo imetolewa wilayani hapa leo na Mtafiti Bestina Daniel kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), wakati akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo ya siku moja kwa maofisa ugani kutoka kata zote na vijiji vya wilaya hiyo.




Alisema ili mafunzo hayo yaweze kuleta maana kwa wakulima na Serikali hawana budi kuyafanyia kazi kwa kwenda kuwafundisha wakulima kwa vitendo mbinu hizo za uzalishaji kwa kuanzisha mashamba madogomadogo ili wakulima waweze kuona na kasha nao kufuata kwa vitendo mbinu hizo pale watakapoona matokeo mazuri kwenye mashamba hayo ya mfano.




“COSTECH kupitia Jukwaa la Bioteknolojia kwa maendeleo ya kilimo nchini (OFAB) wameona waendeshe mafunzo kwa wakagani ambao ndio injini ya kilimo ili kuwakumbusha majukumu yenu na kuwapatia mbinu malimbali ili muweze kukumbuka na kutekeleza majukumu yenu vizuri maana wakulima wanawategemea nyinyi ” alisisitiza Daniel.




Alisema kuwa mafunzo hayo yatalenga kuwapatia mbinu bora za uzalishaji wa mazao ya Pamba,Viazi lishe,Mihogo na nafasi ya matumizi ya bioteknolojia katika kusaidia kupunguza changamoto mbalimbali zinazowakabili wakulima wa sasa na kuongeza uzalishaji.




Kwa upande wake muwakilishi wa ofisa kilimo mkoa wa Tabora, Said Babu alisema Mkoa wao umepata bahati ya pekee kwa wataalamu wake kupata mafunzo hayo ambayo yanalenga kuwaongezea ujuzi na kuwakumbusha majukumu yao.




Aliongeza Mkoa unaamini mafunzo hayo hayatapotea bure na kuishia kwenye ukumbi huo bali wanategemea kuona kilimo cha kisasa kitafanywa na wakulima na kuongeza uzalishaji kwenye msimu ujao wa kilimo kitu ambacho ndicho shabaha ya mafunzo hayo.




Alisema mazao yote matatu ya chakula ya Mahindi,Mihogo na Viazi lishe ni mazao muhimu kwa chakula kwa wakazi wa Mkoa wa Geita hivyo mafunzo hayo yawe chachu mpya katika kufanya mapinduzi kwenye kilimo na kuwataka kutumia mbinu hizo kuzalisha zao la pamba kitaalmu kuwaandaa wakulima na mpango wa serikali ya viwada.




Ofisa Kilimo wa wilaya hiyo ya Uyui, Deogratius Mwampinzi ameipongeza COSTECH na OFAB kwa kuwapelekea mafunzo hayo wataalamu wake kwani mafunzo hayo yatasaidia kuwakumbusha wataalamu hao mbinu walizojifunza vyuoni na kuwapatia mbinu zingine mpya ambazo watafiti wanaendelea kuzigundua ili kuwasaidia wakulima kila siku.




“Tutahakikisha mafunzo haya yanawafikia wakulima kwa kumfuatilia kwenye kata yake kila afisa ugani anayepata mafunzo ili kuona kama mbinu mlizowafundisha zinafahamika na kutumiwa na wakulima”Alissisitiza Mwampinzi.




Hata hivyo amewataka maofisa ugani hao kuwa wasikivu na waulize maswali katika kila mbinu wanayoona inahitaji ufafanuzi ili waweze kuondoaka hapo wakiwa wameelewa vizuri ili wakawaeleweshe wakulima kwenye maeneo yao bila wasiwasi wala kigugumizi.




Mafunzo hayo baada ya kumalizika kwenye wilaya za mkoa wa Geita sasa yanaendelea kwenye Mkoa wa Tabora na wilaya zake ambapo mpaka sasa tayari yameshafanyika kwenye wilaya za Igunga,Nzega na sasa Uyui na yataendelea kwenye wilaya za Sikonge na Urambo

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...