Skip to main content

VIJANA ZAIDI YA 60 WAMLALAMIKIA MUWEKEZAJI KWA KUWARUDHA FEDHA ZAO




wamama wa kijiji cha Sambaru wakiendelea kutwanga mawe kwa ajili ya kuweka tayari kwa kupatikana madini ya ya zahabu


baadhi ya vijana wa kijiji cha sambaru 



Na Woinde Shizza,Singida 


Zaidi ya vijana 60 wa kijiji cha Sambaru kata ya Ikungi wilayani Igungi mkoani Singinda wamemlalamikia mwekezaji wa kampuni ya Sambaru Gold Mining kwa kitendo cha kuwarusha fedha za malipo ya kazi walikuwa wakimfanyia mgodini kwake. 


Wakiongea na waandishi wa habari kijijini hapo baadhi ya vijana hao walisema kuwa wamefanya kazi katika kampuni hiyo kwa kipindi cha mda mrefu lakini muwekezaji huyo ajawalipa ela zao na badala yake amewafukuza kazini hapo bila kuwalipa malipo yoyote .

Mmoja wa vijana hao aliyejitambulisha kwa jina la Saidi Hassan alisema kuwa walishapeleka malalamiko yao kwa viongozi wa kijiji lakini hakuna hatua yeyote iliyochukuliwa hivyo wameiomba serikali iwasaidie ili wapate mafao yao kwani fedha hizo walikuwa wanazitegemea katika kuwasaidia katika majukumu mbalimbali ya kifamilia.


“tumekuwa tunamfata muwekezaji huyu na kumuomba atulipe fedha zetu lakini amekuwa anatukana na kusema atudai ,mbaya zaidi kunawakati alifikia hatua ya kukamata baadhi ya wenzetu ambao wanamdai na kuwapeleka polisi,”alisema Saidi. 

Kwa upande wake kijana mungine aliyejitambulisha kwa jina la Fredy John alisema kuwa kunakipindi walishawahi kumpeleka polisi alipofika na kuulizwa kama vijana hao wanamdai alikuabali na akahaidi kuwalipa na aliomba mda na akapewa kimaandishi lakini ,muda huo umepita na hadi leo vijana hao awajalipwa na amefikia hatua ya kuwakana kabisa.

Gazeti hili lilimtafuta mwenyekiti wa kijiji hicho cha Sambaru Mfaume Hassan ili kubainisha kama anataarifa za vijana hawa nae alisema kuwa ni kweli anataarifa za vijana hawa na alishamtumia mmiliki wa kampuni hiyo taarifa za kuwalipa vijana hawa lakini hajateleza hivyo ameamua kupeleka swala hili katika ngazi za juu ili wamsaidie.  

“sisi kama kijiji tumekuwa tuna utaratibu wa kuwapa vijana wawekezaji hawa na hii inatokana na uhitaji wa muwekezaji ,unakuta muwekezaji anataka vijana wa kumsaidia kazi uko mgodini kwake analeta barua katika ofisi ya kijiji na sisi tunampa vijana na ndio utaratibu uliofanywa sasa muwekezaji huyu kaja kuchukuwa vijana lakini cha kushangaza wamefanya kazi mgodini kwake lakini ajawalipa mpaka leo na mbaya zaidi akifatwa anasema kuwa adaiwi kitu ambacho sio cha kweli mimi kama kiongozi wa kijiji nikishirikiana na wenzangu tutajitaidi kufuata sheria ili vijana hawa walipwe ela zao na hadi sasa navyoongea nilishampa taarifa mkuu wa wilaya”alisema Mwenyekiti wa kijiji Mfaume Hassan.

Gazeti hili lilimtafuta mmiliki wa kampuni ya Sambaru Gold Mining Ahamed Magoma kujibu tuhuma hizi nae alisema kuwa yeye kama yeye adaiwi na kijana yeyote Yule wa kijiji cha Sambaru ,na kama kuna mtu anae mdai afuate vyombo husika vya sheria akamdai.

“mimi sidaiwi na kijana yeyote Yule vijana wangu wote ambao nawaajiri nawalipa vizuri na wengine wapo kazini hadi sasa,pia mimi sijawai kwenda kijijini kutafuta kijana wa kunifanyia kazi na napenda kusema ivi kama kuna mtu ambae ananidai afuate sheria ,aje na vielelezo anidai na kama ni kweli nitamlipa ila sidaiwi na mtu yeyote “alisema Magoma. 

Akiongelea swala hilo mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu alisema kuwa swala hilo alishalipokea kutoka kwa mwenyekiti wa kijiji cha Sambaru na alimuagiza aandike idadi ya vijana hao pamoja na majina yao ili ayafanyie kazi ,aidha pia alisema kuwa atamuandikia barua ya kumuita ofisini kwake mmiliki wa mgodi huo wa Sambaru Gold Mining .












Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...