Skip to main content

DC MTATURU ASIFU UTENDAJI WA MBUNGE ELIBARIKI KINGU


Mbunge wa Jimbo La Singida Magharibi Mhe Elibariki Kingu akizungumza na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Ikungi ulioketi kuchagua viongozi wapya watakaoiongoza jumuiya hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu (Mwenye shati la Njano), Mbunge wa Jimbo la Singida Mgharibi Mhe Elibariki Kingu (Wa Kwanza kushoto Pichani) na viongozi wengine wakifatilia Mkutano Mkuu wa Umoja wa Vijana Wilaya ya Ikungi katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Ikungi.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya Siasa Wilaya akizungumza na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Ikungi ulioketi kuchagua uongozi wapya watakaoiongoza jumuiya hiyo.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Ikungi wakimsikiliza mgeni rasmi katika ufunguzi wa mkutano huo Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu kabla ya kuchagua uongozi wapya kuongoza jumuiya hiyo ngazi ya Wilaya.




Na Mathias Canal, Singida



Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi Mhe Elibariki Kingu ametajwa kama Kiongozi makini anayejali maslahi ya wananchi wa Jimbo, Wilaya, Mkoa na Taifa kwa ujumla katika kipindi kifupi cha utendaji wake tangu alipochaguliwa na wananchi Octoba 25, 2015.


Heko hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati akizungumza na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Ikungi kwenye mkutano ambao ajenda yake kubwa ni uchaguzi wa uongozi wa jumuiya hiyo ngazi ya Wilaya.


Mbele ya wajumbe hao katika Mkutano ulifanyika kwenye ukumbi wa shule ya Sekondari Ikungi Mhe Mtaturu alisema kuwa Mbunge huyo amekuwa mfano wa kuigwa kwani amejikita katika shughuli za maendeleo zaidi katika jimbo lake jambo ambalo linaamsha ari kwa wananchi kushiriki shughuli za maendeleo.


Aliwasihi wananchi kwa ujumla kuendelea kumuunga mkono mbunge huyo kwa ushirikiano wake na viongozi wa serikali za mitaa na Madiwani wa Kata zote sambamba na kumuunga mkoano mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kwa weledi na ufanisi wanaoufanya katika uwajibikaji.


Mhe Mtaturu alisema kuwa Jimbo la Singida Magharibi ndilo pekee katika Wilaya ya Ikungi ambalo limeonekana kuwa katika ramani ya uwajibikaji kupitia mbunge wake tofauti kabisa na Jimbo la Singida Mashariki ambalo maendeleo yake yanasuasua kutokana na chuki za kisiasa.


Aliongeza kuwa Mbunge Kingu amekuwa ni kinara wa kusemea hoja na changamoto za wananchi wa Wilaya ya Ikungi kwa ujumla mara kwa mara katika kipindi chote anapokuwa Bungeni nanje ya Bunge nakuongeza kuwa huo ndio uwakilishi unaotakiwa.


Akizungumza kabla ya kuanza kwa uchaguzi wa viongozi wa jumuiya ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Ikungi Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Mhe Elibariki Kingu alisema kuwa kwa sasa Wilaya ya Ikungi imepata kiongozi imara ambaye anajali maslahi ya wananchi hivyo imani yake maendeleo yatazidi kuimarika kwa wananchi.


Aliwasihi Vijana kushikamana na kuchagua kiongozi bora na si bora kiongozi ili kuendeleza ufanisi wa jumuiya hiyo ambayo ndio muhimili wa Cham Cha Mapinduzi.


Aidha, alisema ataendeleza zaidi ushirikiano baina yake ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu ili kuwanufaisha wananchi na kuboresha zaidi umoja na mshikamano uliopo pasina kuwabagua wananchi kwa itikadi za Chama, Dini ama Kabila.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...