Skip to main content

RC MASENZA ALIOMBA BARAZA LA BIASHARA KUSHIRIKI KIKAMILIFU MAONESHO YA UTALII ...


Mkuu wa Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa Asia Abdallah akitoa maoni wakati wa kikao cha baraza la biashara la mkoa wa iringa juzi, huku mkuu wa mkoa wa iringa amina masenza na mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Iringa Lucas Mwakabungu wakifuatilia kwa makini. (Picha na Friday Simbaya)










Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza (RC) amewaomba washiriki wa baraza la biashara la mkoa kushiriki kikamilifu kwenye maonesho ya Utalii ya karibu Kusini yanayoendelea katika viwanja vya Kichanagni mjini Iringa.

RC alisema hayo juzi wakati wa kikao cha baraza la biashara la mkoa wa Iringa kilichofanyika juzi katika ukumbi wa valentine, kihesa-kilolo mjini Iringa.

Masenza alisema kuwa lengo ni kuufanya mkoa wa Iringa kuwa mfano katika ukanda huo wa kusini katika sekta ya utalii.

Zaidi ya wajasiriamali 350 wamejitokeza kushiriki maonesho ya utalii ya Karibu Kusini yanayoanza rasmi jana, ambayo yatafunguliwa na Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kasimu Majaliwa Kasimu hapo tarehe 29.09.2017 hadi Oktoba 2 katika viwanja vya Kichangani mjini Iringa.

Maonesho hayo yameandaliwa na mikoa ya nyanda za juu kusini kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii, shirika la kuhudumia viwanda vidogo (Sido) na wadau mbalimbali ukiwemo Mradi wa Kuboresha Mtandao wa Maneo Yaliyohifadhiwa Kusini mwa Tanzania (SPANEST).

Alisema kuwa kuna fursa nyingi katika mkoa wa Iringa zinazoanzia katika uwekezaji kwenye sekta ya za utalii ambapo tarehe 29.09.2017 maonesho rasmi ya utalii yatazinduliwa.

“Eneo jingine ni viwanda, biashara, kilimo (maua na matunda), ufugaji, misitu na huduma za kijamii,” alisema.

Aidha, mkuu wa mkoa huyo alisema kuwa mkoa wa iringa umefungua milango na kuowamba wa wakezaji wa ndani na nje kuja kuwakeza baada ya kuweka mazingira wezeshi.

Alisema kuwa wapo wawekezaji wa ndani na nje ambao wamekwisha ziona fursa za uwekezaji zilipo katika mkoa wa iringa na kuzichangamkia.

“Nitoe rai kwa wawekazaji wengine kuzitumia fursa zilizopo. Sisi kama serikali tumejipanga kuwasaidia wawekazaji kutimiza nia yao ya uwekezaji” alisema masenza.

Halmashauri zote katika mkoa wa iringa zimejipanga vema kuwasaidia wawekazji kila wanapojitokeza, aliongezea mkuu wa mkoa huyo.

Awali, mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Iringa Lucas Mwakabungu alisema kuwa kikao cha baraza la biashara la mkoa ni kikao halali kwa mujinbu wa sheria.

Alisema kuwa kikao hicho kinaundwa na wajumbe kutoka sekta ya umma na binafsi kutoka katika mkoa wa Iringa.

Mwakabungu aliwataka wajumbe kutumia fursa katika baraza hilo ndipo vikwanzo na kero zinazokwamisha maendeleo ya viwanda, kilimo na biashara katika mkoa vitatafutiwa ufumbuzi.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...