Skip to main content

DKT TIZEBA AWASIHI VIONGOZI NA WANANCHI KUSHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA CHAKULA


Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles John Tizeba




Viongozi wa serikali, Taasisi binafsi, Wadau wa kilimo, Mifugo na Uvuvi na Wananchi kwa ujumla wake wameombwa kushiriki kikamilifu katika Maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika Katika VIwanja vya CCM Kalangalala Mkoani Geita.


Msisitizo huo umejikita zaidi kwa wananchi wote ambapo umuhimu zaidi umeelekezwa Kwa wakazi wa Mkoa wa Geita na mikoa jirani ukiwemo mkoa wa Mwanza, na Kagera ili kujionea Maonyesho ya kazi mbalimbali zinazolenga kuongeza uzalishaji, tija na upatikanaji wa chakula na usindikaji wa mazao ya kilimo, ufugaji na uvuvi.


Kusikiliza Nyimbo, ngonjera, mashairi na ngoma za asili zinazohamasisha uzalishaji na upatikanaji wa chakula sambamba na Kupata elimu juu ya hifadhi ya mazingira – udongo, maji na viumbe hai.


Akizungumza na waandidhi wa habari Ofisini kwake Jijini Dar es salaam Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles John Tizeba alisema kuwa maadhimisho hayo ya wiki ya chakula ambayo hufanyika kuanzi Octoba 10 mpaka Octoba 16 kila mwaka huwa na dhamira ya Kuwawezesha Wakulima, Wafugaji na Wavuvi kujifunza teknolojia sahihi za kuongeza uzalishaji na tija katika Sekta za Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa lengo la kupata chakula bora na cha kutosha kwa kila mtu na kwa wakati wote.


Alisema ni njia mojawapo kwa wakulima kupata utambuzi wa Kuongeza jitihada na mbinu za kutokomeza njaa, utapiamlo na hatimaye kuondoa umaskini, Kufahamu mikakati thabiti inayoainishwa ya kuhakikisha kila mtu anapata chakula bora na cha kutosha wakati wote, na Wataalamu mbalimbali wa kilimo kuwaelimissha Wananchi ili kuondokana na mila potofu zinazozuia baadhi ya jamii kula aina fulani za vyakula, kwa mfano kutokula mayai kwa akina mama wajawazito.


Dkt Tizeba alizitaja faida zingine za maonesho hayo kuwa ni pamoja na Kuimarisha Ushirikiano wa Kitaifa na Kimataifa katika masuala ya kukuza na kuendeleza kilimo, ufugaji na uvuvi, ikiwa ni pamoja na Kuelezea kihistoria, nafasi ya mila na utamaduni katika kuendeleza sekta za kilimo, ufugaji na uvuvi kwa lengo la kuongeza tija na uzalishaji.


Alisema kuwa Kila mwaka Makao Makuu ya FAO huchagua Kaulimbiu ambayo huwa ndiyo dira ya kuhamasisha wadau wote wa sekta ya kilimo kuchangia katika kuhakikisha kila mtu anawezeshwa kupata chakula bora na cha kutosha wakati wote wa maisha yake.


Kaulimbiu ya mwaka huu inasema “Badili mwelekeo wa uhamaji; Wekeza katika usalama wa chakula na maendeleo Vijijini”.


Kaulimbiu hii inaweka umuhimu katika kuweka Mipango na Programu zinazolenga kuongeza tija na uzalishaji wa mazao ya kilimo na mifugo Vijijini; kupuza utegemezi na kuongeza usawa katika Jamii, sambamba na uhifadhi mazingira ambayo ndiyo muhimu katika maendeleo ya kilimo na hifadhi ya Jamii ili yachochee jitihada za kuondoa umaskini kwa kutumia nguvukazi ya Rasilimali Watu hususani Vijana ambayo imekuwa ikihamia Mijini kwa lengo la kujitafutia mahitaji ya muhimu na mazingira bora.


Chimbuko la Siku ya chakula ni Mkutano wa mwaka 1979 ambapo nchi wanachama wa FAO zilikutana Jijini Quebec nchini Canada na kujadili kiundani masuala mbalimbali kuhusu chakula. Mojawapo ya maazimio ya mkutano huo ilikuwa kutenga siku moja ya kila mwaka ili kuzungumzia na kutafakari njia na mbinu mbalimbali za kupata chakula cha kutosha kwa watu wote duniani na kwa wakati wote.


Maadhimisho ya kwanza ya siku hii yalianza mwaka 1981. Hivyo maadhimisho ya mwaka huu ni ya 36 na yanasherehekewa kwa pamoja na maadhimisho ya miaka 72 ya kuanzishwa kwa FAO tarehe 16 Oktoba, 1945.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...