Skip to main content

Tumbusi hatarini kupotea katika hifadhi za Ruaha na Katavi ikiwa juhudi za makusudi za kiuhifadhi hazitachukuliwa





Wakazi wa Kijiji cha Tungamalenga wilayani Iringa, mkoani Iringa kutoka katika jamii kimaasai wakitumbwiza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Ufuatiliaji wa Tumbusi ndege wala mizoga juzi. (Picha na Friday Simbaya)






Tumbusi ndege wala mizoga wapo kwenye hatari kubwa kutoweka kwa vile idadi yao kubwa wamekuwa wakiuawa kwa sumu na baadhi ya wanavijiji kwa mujibu tafiti zilizofanyika na zinazoendelea kufanyika Afrika mashariki na Afrika kwa ujumla.


Kwa mujibu mratibu msaidizi masuala ya ikolojia kutoka shirika lisilo la kiserikali linalo husika na uhifadhi wa wanayampori (WCS) Iringa Msafiri Mgumba alisema hayo jana katika Siku ya Kimataifa ya Uelimishaji jamii kuhusu Tumbusi, Utafiti unaoendelea kufanyika kwenye eneo la kiikolojia la Ruaha-Katavi unaonesha kuwa changamoto hiyo ipo pia na hifadhi za Taifa za Ruaha na Katavi na Mapori ya Akiba yanayozunguka hifadhi hizo ni eneo muhimu la kiikolojia kwenye uhifadhi wa ndege aina ya Tumbusi..


Hii ni kulingana na utafiti wanaofanya kwa kushirikiana na wataalam kutoka North Carolina Zoo ya Marekani, Hifadhi za Taifa za Tanzania (TANAPA) na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA).

Hata hivyo, Tanzania inaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Uelimishaji wa tumbusi kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi na yaliofanyika katika Kijiji cha Tungamalenga karibu na hifadhi ya Ruaha katika wilaya ya Iringa, mkoa wa Iringa.

Alisema kupitia mpango wa mazingira ya Ruaha-katavi ni muhimu sana katika uhifadhi wa aina 5 za tumbusi ambazo ziko kwenye hatari kubwa ya kutoweka ikiwa juhudi za kiuhifadhi hazitafanyika ikiwa na pamoja na kutoa elimu. Aina hizo za Tumbusi ni kama vile Kichwa Cheupe, Ruppell’s, Mgongo Mweupe, Kichwa Kikubwa na Kapu chini. Aina mbili zipo kwenye hatari ya kupotea lakini siyo hatari kubwa mathalani Tumbusi kichwa kikubwa

Msafiri alisema kuwa katika tafiti za hivi karibuni zinaonyesha kuwa sumu ni tishio kubwa kwa idadi ya ndege wala mizoga hasa katika kwenye maeneo ya uhifadhi wa kijamii/Asasi kama vile Matumizi Bora ya Malihai Tarafa za Idodi na Pawaga (MBOMIPA) na maeneo ya vijiji kuzunguka Hifadhi ya Taifa ya Ruaha (RUNAPA).

Alisema kutokana na uchungaji mifugo mbovu ulipelekea ng’ombe alisahaulika machungani na kupelekea simba kuua, kula na kubakiza. Baadhi ya wafugaji wasiotambua umuhimu wa uhifadhi wa wanyamapori waliweka sumu kwenye mabaki ya mzoga wa ng'ombe alieuwawa na ili kumuuwa simba huyo lakini kwa bahati mbaya kundi la tumbusi walienda kula mzoga huo nakufa, hii ni kutokana kuwa tumbusi anauwezo wa kuona mbali akiwa angani hadi mita 1000 kwa mujibu wa utafiti uliofanyika

Kwa mujibu wa WCS, tumbusi 56 na tai wa kijivu mmoja na ndege wengine aina ya pungu 3 na wanyamapori wengine wanaonyonyesha wawili waliuawa mwezi Mei 2016 kutokana na sumu kwenye eneo la jumuia la MBOMIPA karibu na kijiji cha Tungamalenga kutokana na matumizi mabaya ya sumu kwa baadhi ya wanakijiji wa Tungamalenga katika wilaya ya Iringa, mkoa wa Iringa.


WCS, TANAPA na TAWA wameanzisha kampeni kabambe ya kuelimisha jamii zinazozunguka maeneo ya Uhifadhi kuhusu ndege hao aina ya tumbusi wanaotegemea mizoga kwa kiasi kikubwa kwa sababu baadhi ya wanavijiji hawajui umuhimu wa ndege na sheria za uhifadhi. Kampeni hii inajulikana kama ‘SAIDIA KULINDA TUMBUSI’ kwa manufaa ya wanyamapori, utalii, mazingira na uchumi wa jamii yenyewe na taifa kwa ujumla..


Mwaka 2015 hadi sasa, WCS na North Carolina Zoo wamefanikiwa kuwavisha tumbusi 10 vifaa maalum mgongoni, ili kupata taarifa za mtawanyiko wao, wapi wanaenda na wanapata changamoto zipi, na je wanakwenda kwenye hifadhi nyingine au la. Moja ya matokeo ni kuwa ndege wenye vifaa wameweza kwenda Katavi na Mapori ya akiba mengine karibu na za Katavi na Ruaha na kurudi Ruaha. Tumbusi mmoja ameweza Kutoka Ruaha na kuvuka mpaka wa Tanzania na kwenda hadi Afrika ya kusini. .Tumbusi watatu wa awali waliokuwa wamefungwa vifaa hivyo awali walikufa na inasadikika kuwa ni kutokana na sumu.


Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela aliyekuwa mgeni wa heshima wakati wa Siku ya Kimataifa ya Uelimishaji jamii kuhusu Tumbusi alisema kuwa kuongeza ufahamu kati ya wanakijiji ni mstari wa kwanza wa ulinzi dhidi ya kupungua kwa idadi kutokana na sumu.


Aliwahimiza wanakijiji wasiue ndege hao kwa sababu ni muhimu kwa ajili ya uhifadhi wa mazingira, wanyamapori, watu, utalii na uchumi. 

Kasesela alisema tumbusi hula wanyama waliokufa kwa haraka na kwa ufanisi.

Alisema kuwa matumbo yao yana tindikali yenye uwezo wa kumeng’enya na kuua kabisa vimelea vya ugonjwa kama kimeta, kufua kikuu na kichaa cha mbwa bila wao kudhurika. 


Alisema kuwa uwekaji wa sumu ni kinyume cha sheria kwa mujibu wa sheria ya uhifadhi wa wanayamapori Tanzania ya mwaka 2009 na sheria ya mamlaka ya Usimamizi wa wanyamapori Tanzania 2013 na kuna adhabu kali kwa yeyote aakayeshikwa akitumia sumu kwa lengo la kuua wanyamapori



Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...