Skip to main content

VIJANA WAMPA HEKO RAIS DK. MAGUFULI KWA MAFANIKIO MAKUBWA ...


Polepole akitoa mada kwenye Kambi hiyo

NA MWANDISHI WETU
VIJANA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wametoa tamko la kumpongeza Rais Dk. John Magufuli kwa mafanikio makubwa ya kiutendaji katika utekelezaji wa ilani ya CCM katika kipindi cha miaka yake mwili ya Urais.


Tamko hilo limetolewa katika kambi ya Vijana iliyokuwa ya siku tatu ilijumuisha vijana 500 kutoka Vyuo na Vyuo vya Vikuu nchini na Vijana kutoka Matawi katika Kata zote mkoani Mwanza ikiwa na lengo la kujenga vijana kuwa na uzalendo, maadili bora, uongozi na kuijua vyema itikadi ya Chama Cha Mapinduzi lengo likiwa kuwafanya pia watambue walikotoka walipo na wanakotaka kwenda.


Kambi hiyo ya Vijana iliandaliwa na kuratibiwa na Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu kupitia Seneti ya Vyuo katika mkoa huo.


Akitoa mada, mtoa mada mkuu kwenye kambi hiyo, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole aliwataka Vijana kuwa wazalendo katika taifa lao na kuwataka wasitumike katika kukiharibu chama bali wawe walinzi na wasimamizi wa kukitetea chama na kukosoa watendaji wabovu wanaoiangusha serikali.


Polepole alisema, alisema, vijana wakijengeka katika misingi bora na kuijua vema itikadi ya CCM ndiyo wataweza kuwa na uzalendo, maadili mazuri na kisha kuwa viongozi bora. 


Akisoma maazimio ya kambi hiyo, Katibu wa Vijana mkoa wa Mwanza Mariam Amir alisema, Vijana waliokuwa kwenye kambi hiyo wameazimia kwa pamoja kumpongeza Rais Dk. Magufuli kwa mafanikio makubwa ya kiutendaji wa ilani ya CCM katika kipindi cha miaka yake mwili ya urais na kuahindi kuendelea kumuunga mkono ili kuhakikisha anafanikisha zaidi kusimamia utekelezaji wa ilani ya CCM.


Alisema, wameazimia hivyo kwa sababu Rais Dk. Magufuli katika kipindi hiki cha miaka miwili ameweza kusimamia mambo muhimu ya kuendeleza nchi ikiwemo katika sekta ya elimu, ujenzi wa reli standard geuge, ununuzi wa ndege, ujenzi barabara, bomba la mafuta, makusanyo ya kodi, udhibiti wa upotevu rasimali za umma na nidhamu ya watumishi wa umma.


Mariam alisema Vijana pia wameazimia kuitumikia CCM kwa moyo na nguvu zao zote na kuahidi kuwashughulikia wote wanaokwenda kinyume na maelekezo ya Chama na kutokubali kutumikia mtu zaidi ya kutumikia chama na kuahidi kupeleka ngazi za chini elimu na maarifa ya mafunzo waliyoyapata kutoka kambi hiyo kwa wanachama hasa vijana katika ngazi ya matawi na mashina ili kuendelea kuimarisha itikadi ya chama.


Alipokaribishwa kuzungumza kwa nafasi yake ya Mkuu wa Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu, iliyoandaa kambi hiyo, Daniel Zenda aliwakumbusha vijana wajibu wa kila mwanachama katika kukisemea chama na serikali yake katika mafanikio yaliyotekelezwa kupitia ilani ya CCM


Zenda aliwataka pia vijana nchini kote kupambana kwa vitendo na wale wote wanaojaribu kubeza na kupotosha ukweli kuhusiana na jitihada zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano ya Rais Dk. John Magufuli katika utekelezaji wa Ilani ya CCM.


Alisema umefika wakati sasa wezi na wanaotumia rasilimali za nchi kwa manufaa yao sasa kujondoa weneyewe ndani ya Chama kwa kuwa CCM Mpya imeimarisha misingi yake chini ya Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. John Magufuli na sasa siyo kichaka cha kujifichia wezi.


"Bila shaka mmeshuhudia baadhi wakianza kuondoka wenyewe ndani ya CCM, sasa subirini watazidi kuondoka wezi wengi ndani ya CCM maana kwa sasa hawana namana ya kufanaya zaidi ya kukimbia", alisema Zenda.


Kaimu Katibu wa Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu Ndg Daniel Zenda akizungumza na Vijana katika kambi hiyo.


Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole akitoa mada kwenye kambi hiyo


Vijana katika Kambi hiyo wakinyoosha mikono kuunga mkono maelezo ya Polepole wakati akitoa mada 


Viongozi meza kuu. Kushoto ni Kaimu Katibu wa Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu Ndg Daniel Zenda, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza Anthony Diallo na katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole


Vijana wakikiliza mada


Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela akizungumza na vijana kwenye kambi


Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza, Raymond Mangwala akizungumza kwenye kambi hiyo.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...