Skip to main content

WAZAZI WAASWA KUWASOMESHA WATOTO WA KIKE


Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya Spring Valley iliyoko katika manispaa ya Iringa wakiwa katika mafunzo ya vitendo shuleni hapo.




NA DENIS MLOWE, IRINGA


WAZAZI na Walezi wameaswa kuwasomesha watoto wa kike na kuachana na fikra potofu kuwa kumsomesha mtoto wa kike ni kupoteza rasilimali fedha kwani maisha ya sasa bila elimu ni changamoto kubwa kwa mtoto wa kike.


Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni na Kenneth Komba kutoka Idara ya Elimu mkoa wa Iringa kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza wakati alipokuwa mgeni rasmi wakati wa mahafali ya kumi kidato cha nne katika shule ya Sekondari ya Wasichana ya Spring Valley iliyopo Mkoani Iringa.


Alisema kuwa mtoto wa kike akipatiwa elimu kuna uwezekano mkubwa kwa taifa kuwa na maendeleo kutokana na kuwajibika kwao katika maisha ya kila siku hivyo wazazi na walezi ni muhimu kuwasomesha watoto wa kike kwa lengo la kuendeleza ndoto walizonazo.


Alisema kuwa jukumu la kusomesha elimu ya msingi hadi sekondari ni la serikali lakini wazazi na walezi wanaosomesha shuleni hapo ni kuisaidia serikali hivyo ipo tayari kupokea changomoto zote katika shule hiyo na kushirikiana kuzitatua.


Komba aliipongeza shule ya sekondari Spring Valley kwa kuwa moja ya shule zinazofanya vizuri mkoani hapa kielimu na tabia kwani ni moja ya shule ambazo idara ya elimu haipati malalamiko ya mara kwa mara kutoka shuleni hapo.


Aidha Komba aliwataka wahitimu hao kusoma mazingira ya maisha popote watakapokuwa na kuamua namna ya kujiajiri ili mradi isiwe shughuli zinazopingana na sheria na maadili ya kijamii, kama vile kuuza madawa ya kulevya, ukahaba, unyang'anyi na mambo mengine yanayofanana na hayo ambayo watajiingiza matatani na kuonekana wabaya.

Awali mkuu wa shule ya Wasichana Spring Valley, Adia Mbwanji alisema kuwa uongozi wa shule hiyo umeweka mikakati mbalimbali itakayotekelezwa mwaka 2018 ikiwemo ujenzi wa ukuta upande wa Kusini mwa shule, upanuzi wa maktaba, ununuzi wa gari la shule na kukarabati mifumo ya maji taka na maji safi.


Alisema kuwa shule hiyo inayomilikiwa na kanisa la Baptist Convention of Tanzania imejipanga kujenga chumba cha kompyuta na kununua komputa zenyewe ili kutoa elimu hiyo kwa wanafunzi kuendana na ulimwengu wa sayansi na teknolojia.


Kwa upande wao wahitimu kwa kupitia msoma risala, Happy Njavike walisema kuwa shule hiyo inatakiwa kuboresha ujenzi wa jengo la maabara vifaa vyake vinunuliwe ili kutoa fursa kwa wanafunzi wengi kujifunza kwa vitendo hasa masomo ya sayansi kwa lengo la kukuza ufaulu na kuongeza ujuzi katika masomo ya sayansi.


Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...