Skip to main content

MKUNGA WA KUJITOLEA AMWAGA VIFAA TIBA HOSPITALI YA FRELIMO




Na Friday Simbaya, Iringa 

Mkunga wa kujitolea kutoka Ujerumani ametoa msaada wa vifaa mbalimbali vya tiba katika hospitali ya wilaya ya Frelimo iliopo katika Manispaa ya Iringa, mkoani Iringa. 

Mkunga wa kujitolea, Cornelia Block kwa kushirikiana na taasis ya African foundation for local and international internship (AFLII) ametoa vifaa tiba mbalimbali katika kitengo cha afya ya mama na mtoto, ikiwa ni uzinduzi wa program ya kuchangia vifaa tiba katika hospitali hiyo. 

Alisema kuwa katika awamu ya kwanza ya program ya kuchangia vifaa tiba ametoa vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni tano (5m/-) kwa kushirikiana na shirika la Rainbow Garden Village (RGV) la Ujerumani. 

Block alisema kuwa program hiyo pia itaendesha mafunzo maalum kwa wakunga juu ya mbinu za kisasa za kutoa huduma za afya ya mama na mtoto. 

Alisema kuwa jitihada za kuchangia vifaa tiba zinaendelea ikiwa ni pamoja na fedha kutoka kwa washirika wake ili kupata vifaa tiba zaidi ikiwemo mashine ya ultrasound. 

Hospitali ya Frelimo inakabiliwa na changamoto mbalimbali kama vile jengo la vipimo na uchunguzi, wodi ya kulazwa wagonjwa, wodi ya watoto, wodi ya wagonjwa wa magonjwa ya kuambukiza, jengo la kutakasisha vifaa, jengo la kufulia nguo pamoja na vifaa tiba. 

Naye Mratibu Mkazi wa Taasis ya AFLII Foundation Tanzania, Shedrack Mukuta alisema kuwa taasisi hiyo inaratibu na kuendesha zoezi la kupokea wataalam na wanavyuo wakujitolea wa ndani na nje kwa kuwatafutia nafasi katika vituo mbalmabli vya seriklai na sekta binafsi. 

Alisema kuwa madhumuni makuu ya kuratibu kazi hizo kujitolea ni kusaidiana na serikali na wadau mbalimbali wa maendeleo katika kuboresha huduma za kijamii zikiweo za afya, mazingira, elimu, utalii na uwekezaji kiuchumi. 

Mukuta alifafanua kuwa taasisi hiyo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo katika Mkoa wa Iringa wameweza kupokea na kuwatafutia nafasi za kujitolea bila malipo wataalamu na wanafunzi 47 katika vituo mbalimbali vya serikali pamoja na binfasi. 

Alisema kuwa taasisi hiyo ilisajiliwa mwaka 2016 na kuanza kazi mwaka 2017 katika mikoa ya Mtwara, Zanzibar, Arusha na Iringa. 

Alisema kuwa AFLII Foundation kwa mkoa wa Iringa inafanya kazi na wadau kama vile halmashauri ya Manispaa ya Iringa, Chuo Kikuu cha Iringa, Kanisa la KKKT Dayosisi ya Iringa, Kanisa la Angilikani Dayosisi ya Ruaha, Kibebe Farm na idara za serikali na binafsi. 

Pamoja na jitihada na mafanikio hayo taasisi hiyo bado inakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo mabadiliko katika taratibu na miongozo ya uhamiaji jambo linaloleta usumbufu mkubwa hasa wataalam wanapoingia nchini. 

Kwa upanda wao, mbunge wa viti maalum Mkoa wa Iringa Ritta Kabati (CCM) ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya kukabidhi vifaa vya tiba na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza walimpongeza mkunga wakujitolea Cornelia Block kwa msaada huo. 

Kwa pamoja waliwataka wadau wengine wa maendeleo kujitokeza katika kutatua changamoto katika hospitali ya Frelimo pamoja hospitali zingine mkoani Iringa. 

Walisema kuwa hospitali hiyo inkabiliwa na changamoto ya miundombinu na vifaa tiba ambavyo vimekuwa vikikamisha shughuli za kutoa huduma bora kwa wananchi. 

Hospitali ya Frelimo inahitaji vifaa tiba kama vile biochemistry machine, hematology machine Viral load analyzer, Ultrasound machine na X-ray machine kwa mujibu wa Mganaga Mfawidhi wa Hospitali Dr Pilila Zambi. 


Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...