Skip to main content

OPERESHENI 'NYAKUA NYAKUA' YA NYAKUA DEREVA MKOANI IRINGA




Kandakta wa basi la Rungwe Exprese la kutoka Kyela mkoani Mbeya akikaguliwa kitaba na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Fortunatus Musilimu akiongozana na Mkuu wa usalama barabarani mkoa wa Iringa (RTO) Yusuf Kamotta (Picha na Friday Simbaya)





Na Friday Simbaya, Iringa 

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Fortunatus Musilimu akiongozana na Mkuu wa usalama barabarani mkoa wa Iringa (RTO) Yusuf Kamotta, amefanya ukaguzi wa kushtukiza katika baadhi ya mabasi ya abiria na malori mkoani iringa kwa kukagua liseni za madereva. 


Kamanda Musilimu alikuwa mkoani iringa ikiwa ni sehemu yake ya kufanya ukaguzi wa magari ya abiria pamoja na magari mengine usiku na mchana katika operesheni yake ya  'nyakua nyakua' ya kukamata madereva wanaofanya makosa. 
Operesheni hiyo jana ilifanikiwa kumnyakua dereva mmoja wa mabasi ya New Force mkoani baada ya wananchi kutoa taarifa kuwa dereva huyo alikuwa akiendesha basi  kwa mwendo kasi kwa kuwekwa lupango. 


Hivi karibuni jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, limezindua operesheni 'Nyakua Nyakua' ambayo itahusisha kuwakamata madereva wanaofanya makosa, kuwaweka mahabusu kabla ya kufikishwa mahakamani. 

Kwenye operesheni hiyo, askari wa usalama barabarani hawatawatoza faini madereva watakaokutwa na makosa ikiwamo kuzidisha mwendo na badala yake watawaweka mahabusu na kisha kuwafikisha mahakamani siku inayofuata. 

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, SACP Fortunatus Musilimu, aliliambia Nipashe jana kuwa, operesheni hiyo inafanyika kwa kuondoa mipaka ya kimikoa ambapo sasa askari wa kikosi hicho watakuwa wakishirikiana kukamata madereva wasiotii sheria. 


Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Fortunatus Musilimu akiongozana na Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Iringa Yusuf Kamotta (kulia) akizungumza na abiria wa basi la Rungwe Express wakati wa opersheni yake ya ‘nyakua nyakua’ katika eneo la Igumbilo checkpoint mjini Iringa jana. (Picha na Friday Simbaya)

Kamanda Musilimu alisisitiza kuwa kuanzia sasa madereva wasiofuata sheria za usalama barabarani watanyakuliwa kama mwewe anavyonyakua kifaranga lengo ikiwa ni kudhibiti ajali. 

Musilimu akiwa mkoani Iringa, aliagiza askari wake kuwakamata na kuwaweka mahabusu kisha kuwapeleka mahakamani madereva wote watakaobainika kwenda mwendo hatarishi. 

“Wito wangu kwa madereva wa magari ni kuwa msiipuuzie kauli hiyo, bali muichukulie kwa uzito mkubwa katika kuhakikisha sheria za usalama wa barabarani zinafuatwa ili kuepusha ajali, nyingi zikisababishwa na uzembe wa madereva,” alisisitiza Kamanda Musilimu. 



Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Fortunatus Musilimu akikagua liseni ya mmoja madereva wa malori Paul Chawuya (54) mkazi mjini Ndola nchini Zambia wakati opersheni nyakua nyakua katika eneo la Igumbilo checkpoint mjini Iringa jana. (Picha na Friday Simbaya)



Pia waliwataka madereva wote waende kusoma ili muda utakapofika wa miezi mitano waliopewa na mamlaka madereva wote ambao hatafanya hivyo watafungiwa liseni zao. 

Hata hivyo, kamanda musilimu amewataka askari kuachana na tabia ya kusubiri makondakta kuwapelekea ratiba ya mabasi kwenye vibanda vyao vya kupumzikia lakini askari wanatakiwa kuuingia ndani basi ya kukagua hati zote ndani ya basi huku abiria wanaona. 


Alisema kuwa baada ya kukaa kikao na wamiliki wa mabasi TABOA na kueleza kwamba askari wamekuwa wakichelewesha mabasi walikubaliana kuwa makondakta wasipeleke hati kwenye vibanda vya askari isipokuwa askari aingie ndani ya basin a kukgaua hati zote mbele ya abiria. 

Katika hatua nyingine, kamanda huyo alisema kuwa ili kupunguza malalamiko kuchelewesha ratiba ya mabasi kikosi cha usalama barabarani nchini kwa kushirikiana na TABOA wataainisha vituo maalum vya kufanyia ukaguzi wa mabasi pamoja na magari mengine ili kupunguza utitiri wa vituo vya ukaguzi barabarani. 

Aliongeza kuwa kwa kufanya hivyo kutaongeza ufanisi wa kazi ya ukaguzi pamoja na kuwafanya madereva waendesha magari kuligana na muda uliopangiwa kufika katika maeneo mbalimbali na kufika salama. 


Kwa upande wake, Mkuu wa usalama barabarani mkoa wa Iringa (RTO) Yusuf Kamotta kuwa kuna changamoto ya ajali kwa hivyo amewataka wananchi kufanya ulinzi shirikishi barabarani ili kupunguza ajali. 

RTO Kamotta alisisitiza kuwa ulinzi shirikishi barabarani ni pamoja na kutoa taarifa mapema kabla ya ajali kutokea, na hiyo ndio njia pekee ya kupunguza changamoto za ajali na kuongeza kuwa Tanzania bila ajali inawezekana. 


Hata hivyo, kamanda kikosi cha usalama barabarani nchini SACP Fortunatus Musilumu na mkuu wa usalama barabarani mkoa wa iringa (RTO) Yusufu kamotta waliwashukuru wananchi na madereva kwa kutoa ushirikiano katika kupambana na jail za barabarani. 

Mwisho

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...