Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu
Nchemba, leo Februari 28, 2026 ameshiriki mazishi ya Askofu Mkuu Mstaafu wa
Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, marehemu Mwadhama Polycarp Kardinali
Pengo.
Ibada ya mazishi imefanyika
katika Kanisa la Hija ya Bikira Maria – Pugu, jijini Dar es Salaam, na
kuhudhuriwa na mamia ya waumini pamoja na viongozi mbalimbali wa kitaifa na
kidini.
Mazishi hayo yameongozwa na
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Emmanuel Nchimbi,
ambaye alitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya Serikali na kuwataka Watanzania
kuenzi mchango mkubwa wa Kardinali Pengo katika kulinda maadili, amani na
mshikamano wa taifa.
Viongozi wengine wa Serikali,
wawakilishi wa taasisi mbalimbali pamoja na viongozi wa dini tofauti
walihudhuria ibada hiyo, wakimtaja marehemu kama kiongozi jasiri na mwenye
hekima aliyelitumikia Kanisa na Taifa kwa uadilifu mkubwa.
.jpg)



Comments