Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Benjamini
Sitta, ameipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kwa jitihada zake za
kutoa mikopo kwa wanawake, akisema hatua hiyo imekuwa chachu ya kuwawezesha
wanawake kiuchumi na kuongeza ushiriki wao katika shughuli za maendeleo.
Sitta alitoa pongezi hizo wakati
wa maadhimisho ya Wiki ya Wanawake yaliyofanyika katika Manispaa ya
Iringa, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kuelekea kilele cha Siku ya
Wanawake Duniani kinachoadhimishwa Machi 8 kila mwaka. Kimkoa wa inafanyikia Mji Mafinga.
Alisema mikopo inayotolewa
kupitia halmashauri imewasaidia wanawake wengi kuanzisha na kuendeleza shughuli
mbalimbali za kiuchumi, jambo linalochangia kuboresha maisha ya familia na
jamii kwa ujumla.
Aidha, aliwataka wanawake kutumia vizuri fursa za mikopo wanazopewa ili kujenga uchumi imara na kuleta maendeleo endelevu katika jamii.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa
Manispaa ya Iringa Zaina Mlawa ulieleza kuwa utaendelea kuweka mikakati madhubuti ya
kuwawezesha wanawake, vijana na makundi maalum kupitia mikopo isiyo na riba ili
kuongeza fursa za kiuchumi.
Maadhimisho hayo yalihusisha
shughuli mbalimbali zikiwemo michezo, usafi wa mazingira na kutoa elimu kuhusu
uwezeshaji wa wanawake kiuchumi pamoja na haki zao katika jamii.






Comments