Taarifa za awali zinaeleza kuwa chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika. Hata hivyo, barabara ya mteremko kutoka Kolwezi kuelekea Fungurume inatajwa kuwa hatari na yenye changamoto kubwa kwa magari mazito, hali inayoweza kuwa sababu ya ajali hiyo.
Kwa sasa, eneo la tukio linalindwa na askari wenye silaha kutoka vyombo vya usalama vya DRC, wakiwemo polisi na wanajeshi, ili kuhakikisha usalama wa mzigo uliokuwamo kwenye lori hilo.
Hadi kufikia sasa, hali ya dereva wa lori hilo bado haijathibitishwa.
Taarifa zaidi zitaendelea kutolewa kadri zitakavyopatikana. Wananchi wametakiwa kuendelea kuchukua tahadhari wanapotumia barabara, hasa katika maeneo yenye miinuko mikali.

Comments