Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Fabian Ngajilo, amewafuturisha watoto yatima wanaolelewa katika vituo vya Dar-Bilaal na Dar-Fatma vilivyopo Manispaa ya Iringa, ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za kuwasaidia watu wenye uhitaji katika kipindi cha mfungo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo,
Mbunge Ngajilo aliitaka jamii kuendeleza utamaduni wa kusaidiana na kuwajali
watu wenye mahitaji maalum, hususan watoto yatima, wakati wa vipindi vya ibada
kama Ramadan na Kwaresima.
Alisema vipindi hivyo
vinafundisha upendo, mshikamano na kuwajali wengine, hivyo ni muhimu kwa jamii
kutumia fursa hiyo kusaidia makundi yenye uhitaji ili kuboresha maisha yao.
Aidha, aliwataka wadau mbalimbali
wakiwemo wafanyabiashara, taasisi na wananchi kwa ujumla kushiriki katika kutoa
misaada kwa vituo vya kulelea watoto yatima na watu wengine wenye uhitaji ili
kuwapa faraja na matumaini katika maisha yao.






Comments