Skip to main content

Mtoto (13) Afariki Dunia Akidaiwa Kufanyiwa Ukatili Wa Kingono Iringa


Iringa. Mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 13, mkazi wa Mtaa wa Njiapanda, Kata ya Isakalilo katika Manispaa ya Iringa, amefariki dunia baada ya kudaiwa kufanyiwa ukatili wa kingono.

Mtoto huyo ambaye alikuwa mwanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Zizi, alikutwa akiwa amefariki nje ya nyumba yao, tukio lililosababisha taharuki na huzuni kwa wakazi wa eneo hilo.

Kwa mujibu wa majirani na ndugu wa familia, mwili wa mtoto huyo uligunduliwa asubuhi ya Machi 7, 2026, nje ya nyumba yao baada ya juhudi za kumtafuta kuanza kufanyika kufuatia kutoweka tangu usiku.

Jirani wa familia hiyo, Jacob Mwalongo, alisema walifanya jitihada za kumtafuta mtoto huyo bila mafanikio, kabla ya kutoa taarifa katika kituo cha polisi.

“Tulianza kumtafuta huku na kule lakini hatukumpata. Jioni tulikwenda kutoa taarifa polisi. Asubuhi tulipata taarifa kutoka kwa jirani mmoja kuwa mtoto amepatikana akiwa ameanguka karibu na nyumba. Tulipofika eneo hilo tulikuta tayari amefariki dunia ndipo tukaripoti tena polisi,” alisema Mwalongo.

Jirani mwingine, Adela Issack, alisema walipata taarifa za kupotea kwa mtoto huyo majira ya usiku na wakaanza jitihada za kumtafuta, lakini hazikuzaa matunda.

“Baadaye asubuhi nilipigiwa simu na kuambiwa mtoto amepatikana. Tulipofika eneo la tukio tulikuta mwili wake umefunikwa kwa shuka,” alisema Issack.

Aliongeza kuwa walitoa taarifa kwa askari wa polisi na viongozi wa usalama wa eneo hilo, ambapo uchunguzi wa awali wa mwili ulibaini kuwa mtoto huyo alikuwa na majeraha ikiwemo kuvunjika mkono na shingo kuonekana kulegea, kabla ya mwili kupelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti kwa uchunguzi zaidi.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Njiapanda, Maisha Modestus, alisema tukio hilo ni la kusikitisha na kwamba tayari taarifa zimefikishwa kwa vyombo vya dola ili uchunguzi ufanyike na wahusika wachukuliwe hatua za kisheria.

“Niwahakikishie wananchi kuwa uongozi wa mtaa unaendelea kushirikiana na vyombo vya usalama ili kubaini chanzo cha tukio hili na kuwabaini waliohusika,” alisema Modestus.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, SACP Allan Bukumbi, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi ili kuwabaini na kuwakamata wote waliohusika.

Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Kheri James, akiongozana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, alifika nyumbani kwa wazazi wa marehemu kutoa pole kwa familia na kufuatilia tukio hilo.

RC James alieleza kuwa serikali haitavumilia vitendo vya ukatili dhidi ya watoto na kuagiza Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kudhibiti mara moja uuzwaji wa pombe za kienyeji majumbani, akisema tabia hiyo imekuwa ikichangia matukio ya uhalifu katika jamii.

Alisisitiza kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi ya yeyote atakayebainika kuhusika na tukio hilo.




 

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...