Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Kheri James, amesema kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwigulu Lameck Nchemba, atawaongoza waombolezaji katika mazishi ya kitaifa ya marehemu William Lukuvi.
RC James pia ametoa wito kwa
wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mazishi hayo, akisisitiza kuwa
ni tukio muhimu la kitaifa la kumuaga kiongozi aliyelitumikia taifa kwa muda
mrefu.
Marehemu William Lukuvi aliwahi
kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Watu wenye
Ulemavu).
Akizungumza leo na waandishi wa
habari wakati akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa marehemu kilichopo
Mtaa wa Lukuvi, Kata ya Gangilonga, Manispaa ya Iringa, Kheri James alisema
serikali imeandaa mazishi hayo kwa hadhi ya kitaifa na inatarajia ushiriki
mkubwa wa waombolezaji.
Aliongeza kuwa mazishi hayo yatafanyika katika Kijiji cha Idodi, Jimbo la Isimani, Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, ambapo viongozi mbalimbali waliopo madarakani pamoja na waliostaafu wanatarajiwa kuhudhuria shughuli hiyo ya mwisho ya kumuaga marehemu.



Comments