Wajasiriamali hao walisema maadhimisho hayo yamekuwa jukwaa muhimu la kutangaza biashara zao, kupata wateja wapya na kubadilishana uzoefu wa kibiashara, jambo linalochangia kuwawezesha zaidi kiuchumi.
Baadhi ya wajasiriamali
walioshiriki ni pamoja na Happy Home Decor na Mwanamke Glow Skincare, ambao
walitumia nafasi hiyo kuhamasisha wanawake kujitegemea kiuchumi badala ya
kutegemea wanaume kwa kila jambo.
Walisema mwanamke anapokuwa na
shughuli ya kiuchumi inayomwingizia kipato, huongeza uwezo wa kujitegemea,
kuchangia maendeleo ya familia na jamii kwa ujumla.






Comments