Skip to main content

POLISI IRINGA WAKAMATA WATUHUMIWA 53, WAONYA TAARIFA ZA UONGO



Na Friday Simbaya, Iringa

Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa limekamata jumla ya watuhumiwa 53 kwa makosa mbalimbali ya uhalifu katika operesheni zilizofanyika maeneo tofauti kuanzia Aprili Mosi, 2026, huku likitoa onyo kali kwa wananchi dhidi ya utoaji wa taarifa za uongo zinazosababisha taharuki.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, SACP Allan Bukumbi, alisema miongoni mwa waliokamatwa ni Ramadhani Mussa (33), dereva mkazi wa Dar es Salaam, aliyetiwa hatiani kwa kosa la kutoa taarifa za uongo kuwa ameibiwa sehemu zake za siri.

Kwa mujibu wa Bukumbi, mahakama ilimhukumu Mussa kifungo cha miaka mitano jela baada ya kuthibitika kuwa taarifa aliyotoa haikuwa ya kweli.

“Katika operesheni hizi, tumefanikiwa pia kuwakamata watu wengine waliokuwa wakitoa taarifa za uongo na kusababisha taharuki kwa wananchi,” alisema Bukumbi.

Aliwataja watuhumiwa wengine kuwa ni Mussa Kaundi (39), mfanyabiashara mkazi wa Mafinga, pamoja na wenzake wawili kutoka Isakalilo, Manispaa ya Iringa, na Usokami, Mafinga, ambao kwa nyakati tofauti walidai kuibiwa sehemu zao za siri.

Alieleza kuwa uchunguzi wa kitabibu ulithibitisha madai hayo hayakuwa ya kweli, huku upelelezi wa kesi hizo ukiwa umekamilika na watuhumiwa wakitarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.

Katika hatua nyingine, Kamanda Bukumbi alisema Jeshi la Polisi linaendelea kutoa elimu kwa madereva wa vyombo vya moto na watumiaji wengine wa barabara kuhusu umuhimu wa kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani.

Alisema baadhi ya madereva wamechukuliwa hatua za kisheria kutokana na makosa ya barabarani, ikiwa ni pamoja na kufungiwa leseni.

Aliwataja madereva hao kuwa ni Efes Ndembela, aliyefungiwa leseni kwa miezi mitatu kuanzia Aprili 8, 2026, baada ya kukutwa akiendesha basi lenye namba T249 DYD aina ya Zhongtong, mali ya kampuni ya New Force Enterprises, kwa mwendo kasi katika eneo la Iyovi.

Mwingine ni Ally Mbwilo, aliyefungiwa leseni kwa miezi mitatu kuanzia Aprili 10, 2026, kwa kosa la kuendesha basi lenye namba T840 DUS aina ya Fuso, mali ya kampuni ya Alimwene, kwa mwendo kasi akiwa njiani kutoka Iringa kuelekea Ruaha Mbuyuni.

Jeshi la Polisi limetoa wito kwa wakazi wa Iringa na wananchi kwa ujumla kuacha kujihusisha na vitendo vya uhalifu na upotoshaji wa taarifa, na badala yake kushirikiana na vyombo vya dola ili kudhibiti vitendo hivyo mapema.




 

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...