Skip to main content

TFS YASISITIZA MAADILI KAZINI, YATAKA UZINGATIAJI WA MATUMIZI SAHIHI YA MIFUMO

Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi TFS na Meneja wa Rasilimali Watu, Bahati Mtomaye alisema kuwa matumizi sahihi ya Mifugo pamoja na kuzingatia maadili ni nguzo muhimu katika kuboresha utendaji wa taasisi na kujenga imani kwa umma
Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi TFS na Meneja wa Rasilimali Watu, Bahati Mtomaye alisema kuwa matumizi sahihi ya Mifugo pamoja na kuzingatia maadili ni nguzo muhimu katika kuboresha utendaji wa taasisi na kujenga imani kwa umma.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya matumizi sahihi ya mifumo katika utendaji.



Na Fredy Mgunda, Mufindi


WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) umeanza kuonyesha msimamo mkali katika vita dhidi ya rushwa na ukiukwaji wa maadili kwa kuwataka watumishi wake kuzingatia kikamilifu nidhamu ya kazi na matumizi sahihi ya mifumo ya kiutumishi, hatua inayolenga kuongeza uwajibikaji na ufanisi katika utendaji.


Msisitizo huo umetolewa katika siku ya pili ya semina ya mapambano dhidi ya rushwa na maadili kwa maafisa na askari wa Shamba la Miti Sao Hill, mkoani Iringa, ambapo watumishi wamekumbushwa wajibu wao wa kulinda rasilimali za umma kwa uadilifu.


Semina hiyo imewakutanisha watumishi wa TFS kwa lengo la kuimarisha uelewa wao kuhusu wajibu wa utumishi wa umma, hasa katika kuzingatia misingi ya uwazi, uadilifu na uwajibikaji wanapotekeleza majukumu yao ya kila siku.


Katika mafunzo hayo, washiriki wameelekezwa kwa kina juu ya umuhimu wa kufuata sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma, sambamba na matumizi sahihi ya mifumo ya kiutumishi ikiwamo Mfumo wa Upimaji Utendaji Kazi (PEPMIS), unaolenga kuongeza uwazi, ufanisi na ufuatiliaji wa utendaji wa watumishi.


Akizungumza katika semina hiyo, Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi TFS na Meneja wa Rasilimali Watu,  Bahati Mtomaye, alisema matumizi sahihi ya Mifugo pamoja na kuzingatia maadili ni nguzo muhimu katika kuboresha utendaji wa taasisi na kujenga imani kwa umma.


“Ni muhimu kwa kila mtumishi kuzingatia maadili ya kazi na kutumia mifumo ya kiutumishi kama inavyotakiwa, kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa ili kuongeza uwajibikaji,” alisema.


Hatua hiyo ya TFS inakuja wakati Serikali ikiendelea kusisitiza uwajibikaji na mapambano dhidi ya rushwa katika taasisi za umma, huku ikitaka watumishi kuwa mstari wa mbele katika kulinda rasilimali na kuhakikisha huduma bora kwa wananchi.


Semina hiyo inaendelea kuwa kichocheo cha mabadiliko chanya kwa watumishi wa TFS katika Shamba la Miti Sao Hill, ikilenga kujenga utamaduni wa uwajibikaji, uadilifu na utendaji unaozingatia matokeo.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...